Ben Pol msanii wa bongo flavor na mshindi wa tuzo za muziki za Kilimanjaro kwa mwaka 2011 na 2012 akiwa na bango la 'Boresha Chekchea'. |
Ule usemi wa kuwa msanii ni kioo cha jamii unajidhirisha kwa msanii wa mziki wa bongo flavor Bernard Michael Paul Mnyang'anga anae julikana kisanii kama Ben Pol kuunga mkono kampeni ya kuboresha elimu ya awali Tanzania.
Kampeni hiyo ilizinduliwa na HakiElimu tar 27 September 2012 iliyoambatana na uzinduzi wa matangazo mawili ya Television na redio kwaajili ya kuendeleza kampeni hii ya elimu ya awali iliyopewa jina la Chekechea.Matangazo hayo yanaonesha changamoto
zilizoko katika elimu ya awali nchini na kutoa mfano wa shule
bora au elimu ya awali inayotakiwa nchini Tanzania.
Ben Pol akiwa katika baadhi ya kazi zake za kisanii jukwaani |
Elimu
ya Awali ni muhimu kwa maendeleo ya mtoto kimwili, kiakili na kimaadili. Katika
Sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 1995 Serikali inaonesha umuhimu wa elimu ya
awali,inapotamka ; “Tafiti kadhaa zilizofanyika
nchini katika miaka ya 1980 zilibaini kuwa watoto waliopitia elimu ya awali
huwa na mafanikio makubwa zaidi wanapoanza darasa la kwanza. Kutokana na
kutambua umuhimu huu, Serikali iliamua kuingiza Elimu ya Awali kwa watoto wenye
umri wa miaka 5 na 6 kwenye mfumo rasmi wa elimu na kila shule ya msingi
inapaswa kuwa na madarasa ya Elimu ya Awali.”
Sera ya Elimu na Mafunzo 2010. Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi . Toleo jipya Rasimu ya 2 March 2011.(uk 5-6).
Uwekezaji katika huduma bora kwa
mtoto na elimu ya awali huwa na faida maradufu kwa watoto wetu- ambao ni raia wetu wa baadaye. Walipa kodi nao pia hufaidika na
huimarisha uchumi. Faida ya uwekezaji wa fedha za umma katika elimu bora ya
awali ni kubwa sana. Lakini je, Tanzania imeligundua hili na
kulitekeleza kikamilifu? Na je, maneno
haya ambayo sera inasisitiza yako yanatekelezwa kwa vitendo?
0 comments:
Post a Comment