Maoni ya Wadau wa Elimu kuhusu Bajeti ya Wizara ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi iliosomwa Bungeni 13 Agosti, 2012 - HakiElimu, Dar es Salaam.
HakiElimu inalitazama
suala la elimu kwa kila mtu kama haki ya msingi baada ya haki ya kuishi, kwetu
sisi elimu ndiyo haki pekee inayoweza kumsaidia mtoto au mwanadamu yoyote aweze
kupata haki zake nyingine zote. Kwa sababu hiyo, HakiElimu inaamini kuwa suala
la kupambana na changamoto zinazoikabili sekta ya elimu nchini si la kufumbiwa
macho na ni jukumu la kila Mtanzania.
Kama shirika
linalojihusisha na utetezi wa haki ya kupata elimu, HakiElimu iliandaa na
kufanya mkutano na wadau wa elimu mbalimbali uliyolenga kujadili hali ya elimu
nchini, kufuatilia Bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya 2012/2013,
ikiwasilishwa Bungeni tarehe 13 Agosti,
2012 na kutoa maoni, mitazamo na ushauri juu ya bajeti hiyo na mwelekeo wa
elimu kwa ujumla.
1. Katika
hotuba yake Waziri hajazungumzia kabisa mgomo wa walimu uliofanyika hivi
karibuni. Hii inatia shaka kama serikali ina nia ya dhati kushughulikia kero na
matatizo ya walimu. Kama serikali inataka kufikia muafaka na walimu na
kuboresha ufundishaji ni lazima ikubali kuwa kuna tatizo na isikwepe wala kuona
aibu kulijadili suala hili kwa uwazi. Aidha, Bajeti haina mkakati maalumu wa
kuongeza ubora wa walimu ambao ni muhimu katika kuleta elimu bora. Serikali
imeendelea kupuuza maslahi ya walimu huku ikikataa kukubali kuwa bila
kukuboresha maslahi yao hawatafanya kazi kwa moyo.
2. Waziri
pia hakugusia vizuri suala la migomo ya wanafunzi vyuo vikuu ambayo mingi
husababishwa na matatizo ya Bodi ya Mikopo. Ni muhimu kubadilisha mfumo wa
utoaji wa mikopo; Bodi ya Mikopo iwe na matawi mikoani ili kurahisisha utoaji wa
mikopo na kupunguza urasimu. Pia, katika kupunguza kero zilizopo kwa wanafunzi
wasiokuwa na uwezo wa kujilipia masomo ya juu, Serikali ingekuja na mkakati wa
kuwasomesha wanafunzi waliofaulu kwa kiwango cha juu. Hii ingekuwa tumaini kwa
watoto wanaotoka kwenye familia masikini.
3. Bajeti
hii haina tofauti yoyote na ile ya mwaka jana kwa maana ya uwezo wa kutatua changamoto
za elimu na hatutegemei mapya katika utekelezekaji wake. Bajeti haizungumzii
kwa kina jinsi ya kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya elimu; haina
upembuzi yakinifu wa matatizo na njia za kuyatatua.
4. Bajeti
bado inatoa kipaumbele katika matumizi ya kawaida na kupuuza uwekezaji wa
msingi katika elimu. Mathalani, katika makadirio ya bajeti ya takribani
shilingi bilioni 724, ni shilingi bilioni 92.5 tu zilizotengwa kwa ajili ya
shughuli za maendeleo katika elimu. Hii ina maana kuwa ni asilimia 13 ya bajeti
itaenda kwenye shugghuli za maendeleo na zaidi ya bilioni 630 (87%) zimekwenda
katika matumizi ya kawaida!
5. Aidha,
suala lingine lililojitokeza ni utegemezi mkubwa wa Serikali kwa fedha za
wahisani katika kutekeleza miradi yake ya maendeleo. Katika Bajeti hii kati ya
shilingi bilioni 92.5 zilizotengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo, ni
shilingi bilioni 18.5 (asilimia 20) tu ndizo zitatoka katika vyanzo vya ndani
wakati shilingi bilioni 74 (asilimia 80) zinatarajiwa kutoka kwa wahisani!
Utegemezi kwa wahisani wa kiwango kikubwa hivi ni hatari kwa maendeleo ya nchi
yetu kwani kama wahisani hao watakwama kutoa misaada yao basi mipango yetu ya
maendeleo nayo itakwama
6. Tumemsikia
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akisema uwiano wa mwalimu kwa wanafunzi
umeboreshwa kutoka 1 kwa 48 hadi 1 kwa 46. Kwa juu juu, inaonekana tumefanya
vizuri, kwani lengo letu ni kufikia uwiano wa 1 kwa 45. Lakini kuna angalizo; huu
ni wastani na unaficha ukweli kwamba katika maeneo mengi watoto wanaweza kuzidi
50, 60 au 70 kwa mwalimu mmoja. Bajeti ikijaa maelezo yanayojikita kwenye kutoa
wastani bila ufananuzi kuhusu hali halisi ni hatari sana kwani haitoi taswira
halisi ya ama kukua, kudumaa au hata kudorora
kwa elimu nchini.
7. Waziri
ameahidi kwamba katika kipindi cha 2012/13, Wizara yake itaifanyia kazi sera
mpya ya elimu; lakini, hajasema ni lini sera hiyo itakuwa tayari. Tunasistiza
umuhimu wa kutimiza ahadi hii mapema kwani sera hii ndiyo itaongoza utoaji wa
elimu Tanzania. Sera ya 1995 imepitwa na wakati na sasa ni serikali inapaswa ije na sera mpya inayozingatia mabadiliko ya
kiuchumi na dira ya maendeleo.
8. Serikali
imeendelea kutoa ahadi juu ya mpango mpya wa maendeleo ya elimu ya msingi awamu
ya tatu baada ya ule wa awamu ya pili kumalizika 2010, lakini haielezi
maandalizi yamefikia hatua gani na lini utakuwa tayari. Ni vema serikali
ikaharakisha mpango huo ili kutoa dira kwa watekelezaji wa sera na bajeti za
kila mwaka.
9. Hotuba
ya Waziri imeendelea kupuuza matatizo katika shule za kata hasa suala la kutokuwa
na mabweni. Kuna athari nyingi sana za kuwa na shule umbali mkubwa kutoka
makazi ya wanafunzi. Hii ni pamoja na wasichana kuwa hatarini kupata mimba n.k.
Serikali haijasema wala kuonesha mkakati madhubuti wa kuyafanyia kazi matatizo kama
haya.
10. Alipokuwa
akiongelea suala la ubora, Waziri alijikita zaidi katika kuongelea namna Wizara
ilivyoboresha matokeo katika mtihani wa kuhitimu shule ya msingi, kutoka
asilimia 53.5 hadi 58.3. Wakati kweli hili ni ongezeko, bado haliridhishi. Aidha,
kumekuwa kuna tatizo kubwa sana kwenye ufaulu wa mtihani wa kuhitimu kidato cha
nne kwani asilimia 90 ya waliofanya mtihani huu mwaka jana walipata div 4 au 0.
Utoaji wa elimu bora ya sekondari utaisadia sana Tanzania kufikia malengo yake
ya maendeleo kwani mwananchi anayeipata atakuwa na uwezo mkubwa wa kulinda afya
yake, kujiendeleza kiuchumi na kujitambua. Hivyo, tunashangazwa na kushtushwa
na ukimya wa Waziri kuhusu suala hili.
11. Wakati
tunatarajia kuandaa sera mpya ya elimu ni vema pia tukatafakari kuhusu suala la
lugha ya kufundishia. Wakati ni muhimu kwa Mtanzania wa karne hii kukijua
Kiingereza na ufundishaji wa lugha hii lazima uboreshwe, ni muhimu zaidi kuwafundisha
watoto kwa lugha ambayo wanaielewa ili wapate ujuzi.
12. Mwisho,
wakati Wizara inapanga mikakati yake, ni muhimu kuwa na mpango madhubuti kuhusu
wahitimu kwani kundi hili likikata tamaa kutokana na kushindwa kupata ajira
n.k., linaweza kuleta mtikisiko mkubwa katika taifa.
Education
stakeholders’ response to the Ministry of Education and Vocational Training
budget reading on 13th August 2012 – HakiElimu, Dar es Salaam.
HakiElimu’s vision is to see
an open, just and democratic Tanzania, where all people enjoy the right to education
that promotes equity, creativity and critical thinking. We believe that for
this to happen, people need to be involved in shaping the country’s public
education system at all levels.
This is why on August 13,
2012, HakiElimu brought together various stakeholders to discuss the state of
education, listen to the reading of the Ministry of Education and Vocational
Training 2012/2013 budget and discuss how effectively it addressed their
varying concerns. The meeting was held on the premises of REPOA in Dar es
Salaam and culminated in the following recommendations and concerns:
1. It was
surprising that the Minister made no mention of the teacher’s strike. For many
around the country, this was one of the most significant events in the
education sector this year. By not speaking about it, the Ministry and
Government gave the public the impression that they are not interested in
improving teachers’ welfare. If the Ministry hopes to improve learner outcomes,
it must be open and transparent in dealing with teachers’ concerns and these
must be prioritised in the quest for quality education.
2. The
minister’s budget speech failed to highlight enduring strikes by students in
higher learning institutions as a challenge. These strikes are most often
caused by students’ dissatisfaction with the higher learning loans system and
might be significantly reduced if the system was decentralized so that the
Loans Board worked through offices at regional level. Government should
introduce a scholarship system so that students who distinguish themselves
through their performance are assured that their studies will be paid for. This avenue would provide hope to students
from poor families.
3. This
budget is no different than last year’s budget in terms of how it will address
current challenges in the education sector; we don’t expect anything new as a
result of its implementation. The budget does not discuss at length strategies
that will be used to address education sector challenges, it does not
critically analyse underlining issues and concerns.
4. This
year’s budget continues to privilege recurrent over development expenditures
thus neglecting the opportunity, yet again, to invest in education. Out of an
estimated expenditure of approximately 724 billion shillings, just 92.5 billion
has been budgeted for development efforts. In contrast, over 630 billion
shillings has been allocated for recurrent expenditures.
5. Another
issue that emerged had to do with the Ministry’s dependency on funds from
development partners in order to implement development projects. In this year’s
budget, out of the 92.5 billion shillings allocated to development projects,
just 18.5 billion or 20 per cent will be generated from internal or local
revenue sources. The rest, which is 74 billion shillings or 80 per cent of the
development budget, is expected to be financed by development partners. This
level of dependency on external sources is worrying given that development partners sometimes renege on
commitments to make funds available.
6. In his
speech the Minister of Education and Vocational Training mentioned the
improvement in teacher-pupil ratio, from 1 to 48 to 1 to 46. On the surface, it
would appear we have done well in this area, given that our objective is to
have at least 1 teacher to 45 pupils. But in reality, the figure given is an
average and across the country there are classrooms with over 50, 60 and even
70 pupils to one teacher. The use of averages in presentations such as this one
without further explanation is misleading and consequently fails to provide the
public with a real picture of what is going on in education.
7. The
Ministry expects to finalise the new education policy document during this
financial year, although it has not said specifically when. We would like to
urge the Ministry to make sure that this happens because the 1995 education and
training policy is out of date. It is important that the government finally
releases a new policy that takes into account changes in the economic context
and development vision of the country.
8. The
Government, through the Ministry of Education and Vocational Training,
committed itself to implementing a third phase of the primary education
development programme, after the second phase came to an end in 2010. We urge
the Government to ensure that this programme is ready for implementation and
that it carries a vision for the positive transformation of primary education
in Tanzania.
9. The
budget speech continued in the tradition of underestimating the challenges that
community secondary schools are facing, and particularly the lack of hostels at
these schools. There are several cons to having schools located at a long
distance from where learners and their communities live; it is particularly
dangerous for girls and increases the incidence of schoolgirl pregnancies and
other undesirable situations. The Ministry failed to clearly explain how it
will work to address challenges such as these in the coming financial year.
10. When
discussing the issue of education quality, the Minister focused on how the
Ministry had successfully raised the primary school pass rate from 53.5 to 58.3
per cent. While this is indeed an improvement, it is still not satisfactory and
more needs to be done to improve learner outcomes. This is particularly urgent
at secondary school level, where in the most recent form four exams, 90 per
cent of the examination candidates record a dismal performance of division four
or zero. The provision of quality secondary education is fundamental to the
development of this country because of its potential impact on human
development and particularly in the areas of health and citizen agency. We are
shocked and surprised that the Minister failed to mention this.
11. While
the Ministry undertakes to finalise and release a new education policy, it is
important that the issue of language of instruction is finally addressed. While
it is important for Tanzania’s to become competent users of the English
language, and teaching of this language in our schools must improve, our
priority should lie in ensuring that learners are taught in a language that
they understand and that can impart them with the skills they need.
12. Finally,
as the Ministry develops its plans and strategies, it is important that it
comes up with a strategy for addressing the high levels of youth unemployment as
if the current situation continues
unchecked, it could lead to civil disturbance and unrest.
0 comments:
Post a Comment