Tuesday, August 7, 2012

Uwekezaji katika elimu ya awali hauepukiki. Serikali ichukue hatua

Wanafunzi wa darasa la awali katika shule ya msingi misunkumilo wilayani nkasi wakirudi nyumbani baada ya masomo.





Elimu ya awali ni muhimu sana hasa kwasababu ni msingi mzuri katika kumtayarisha mtoto kuanza kukabiliana na changamoto za elimu hasa elimu ya msingi kwani humtayarisha mtoto ili kuanza kupenda elimu na hivyo kufanya vyema katika ngazi zinazofuata za elimu kuanzia msingi, sekondari na elimu ya juu.

Kuona umuhimu wa elimu ya awali, Tanzania ilianzisha mfumo wa elimu unaotaka kila shule ya msingi kuwa na darasa la awali ili kuandaa watoto wa watakaoingia darasa la kwanza.Watoto hawa huandikishwa elimu ya awali wafikapo miaka mitano au sita ili wafikapo miaka saba wanaaza darasa la kwanza.

Uwekezaji kama huu ni wa kukatisha tamaa katika elimu.Darasa la awali katika shule ya msingi Selous wilayani Namtumbo
Hii ni hatua muhimu sana na kama uwekezaji wa kutosha utafanyika, basi tanzania siku moja itashuhudia ukuaji mkubwa wa kiwangio cha elimu. baadhi ya nchi za Afrika zinazofanya vyema sana katika elimu ya awali ikianzia miaka mitano ya toka mtoto anazaliwa (Early Childhood Education) ni Nigeria,Afrika ya kusini na Ghana ambazo zimewekeza vilivyo katika elimu ya awali (watoto) na matokeo yake yamezifanya nchi hizi kuwa na viwango vya juu vya elimu Afrika nzima.

Ripoti ya mwaka huu (2012) ya Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (Unicef) kuhusu hali ya watoto, inaonesha dhahiri umuhimu wa elimu ya awali katika kupunguza watoto wa mitaani.zaidi ya watoto milioni 200 kutoka nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania hushindwa kutumia fulsa za elimu ipasavyo kutokana na mifumo mibovu ya elimu ya awali. 
 

Hivyo, uwekezaji wa kweli unaozingatia upatikanaji wa huduma muhimu kwa watoto wote ili kutoa fursa sawa ya kujiendeleza na kuweka misingi ya watoto kupenda kusoma ni muhimu sana ili kuinusuru elimu ya Tanzania.

Hivi karibuni ililipotiwa na vyombo vya habari kuwa zaidi ya wanafunzi 5,000 waliofaulu na kujiunga na kidato cha kwanza walibainika kutokujua kusoma na kuandika hali inayolalamikiwa kuwa chanzo chake ni uwekezaji mdogo katika shule za msingi inayoanzia na elimu ya awali.






0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More