Friday, August 10, 2012

Je Bajeti ya Elimu 2012/2013 itaboresha mazingira ya shule kama hizi.








Shule hii ipo wilayani Muleba mkoani Kagera.
Ndani ya shule hii licha kuwa ni shule yenye kuta na kuezekwa kwa nyasi, 
bali pia wanafunzi wanakaa chini
Shule ya msingi Silabu wilayani Korogwe.Wanafunzi hawa wanasoma kwenye kichochoro
 kilichopo katikati ya madarasa mawili

 Shule ya msingi Silabu wilayani Korogwe.

Shule ya msingi Selous iliyopo wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma.



 Bajeti ya elimu itasomwa bungeni siku ya Jumatatu, 13 Agosti. Wakati bajeti ya Elimu inasubiriwa kwa hamu na wadau na hasa wapenda maendeleo ya Elimu, Baadhi ya maeneo nchini bado yanakabiliwa na changamoto kubwa sana hasa hali mbaya ya miundombinu, ukosefu wa vyumba vya madarasa na majengo ya shule ambayo yamesababisha baadhi ya shule kuweka madarasa ya nyasi kama shule ya msingi Selous na Mkapa zilizopo wilayani Namtumbo, Shule ya msingi Silabu iliyoko wilayani Korogwe, Shule ya msingi Misunkumilo ya wilayani Nkasi, na baadhi ya shule wilayani Muleba.

Hali ya elimu imezidi kuwa mbaya kila kukicha, kiasi kwamba hata watu hudiriki kuuliza kama shule hizo zipo nchini, hasa wakiangalia juhudi na kelele nyingi zilizopigwa juu ya mchango mkubwa wa MMEM na MMES kuwa zimefanya kazi kubwa sana kuboresha mazingira ya kujifunzia hasa miundombinu ya shule.Swali Je, shule hizi ziliachwa wapi na mipango hii? Je bajeti ya elimu ya 2012/2013 itatatua baadhi ya changamoto za elimu nchini?na kuondokana na majengo haya yasiyo rafiki kwa mwanafunzi na mwalimu?

 Mwana blog ya HakiElimu, Hebu angalia jinsi ambavyo wanafunzi huko Tanga,Rukwa,Kagera na Ruvuma wanavyojifunza kwenyesehemu zinazokatisha tamaa : Watatoka?


Shule ya msingi Selous iliyopo Namtumbo. Wanafunzi wa darasa la tano wakiwa darasani 
na mwalimu akifundisha.
  
Wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya Isensa ya wilayani Nkasi wakiwa darasa, darasa hili lina wanafunzi 211, mwalimu hana pa kukaa akifundisha hutoka nje kusubiri watoto wamalize kuandika.

Wanafunzi wa shule ya msingi Misunkumilo ya wilayani Nkasi wakisoma kwenye darasa lililoezakwa kwa turubai, shule hiyo ina madarsa mawili ya namna hiyo ambayo yanatumiwa na wanafunzi wa darasa la tatu, la nne na awali.
Shule hii ipo wilayani Muleba.
Hiki ni choo cha shule wilayani Muleba

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More