Thursday, June 21, 2012

Miundombinu ya shule ni kikwazo kwa watoto wenye ulemavu kupata elimu Musoma


 Rajabu Josephat  mwanafunzi mwenye ulemavu wa miguu katika shule ya  Msingi
Nyankanga na Pius Ligamba wa shule ya Secondary Kemoramba.
Mazingira yasiyo rafiki mashuleni yamesemwa kuwa chanzo cha watoto wenye ulemavu kutoandikishwa shule na waliokwisha andikishwa kuacha shule kutokana majengo ya shule ambayo yamejengwa bila kuzingatia mahitaji ya wanafunzi wenye ulemavu wa viungo.
Utafiti mdogo wa kihabari uliofanywa na jopo la waandishi wilayani Musoma vijijini, ulionesha kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwaficha watoto wenye ulemavu majumbani na kutoamua kuwapeleka shule kutokana na kukwepa watoto wao wasipate tabu au hata kupata magonjwa ya kuambukiza wakiwa shule.

Pius Ligamba Mwanafunzi wa shule ya msingi Kemoramba wilayani Musoma

Shule ya sekondari Kemoramba, Shule ya msingi Nyankanga na Shule ya msingi  Mmahare ni baadhi ya shule zilizotembelewa na kuonekana hazina miundombinu ya majengo rafiki ili kuwezesha wanafunzi wenye ulemavu kusoma bila matatizo makubwa.

Shule nyingi wilayani musoma vijijini hazina majengo yenye kujali mahitaji ya walemavu wa viungo wala hawana mipango ya karibuni ya kutengeneza miundombinu kwaajili ya walemavu.
 
Mkazi mmojawapo wa kijiji cha Nyankaga bwana  Mr Wekesa Nyamarwa,  alimwambia mwandishi wa habari hii kuwa mototo wake ambaye ameshapitisha umri wa kwenda shule alichagua kutokumuandikisha ili kumuepusha na mazingira hatarishi na mabaya ambayo anasema yasingemuwezesha mtoto wake kufuatilia vyema masomo yake.

Bwana Nyamarwa anajua mtoto wake atapata matatizo makubwa akiwa shuleni na katika masomo yake ambayo yatamchanganya na kumfanya aache shule bila kufikia malengo yake aliyojiwekea.Alitoa mfano wa shule ya msingi Nyakaga kuwa haina miundombinu inayoweza kumfanya mlemavu ajisikie nae kama wanafunzi wengine.
Bwana Nyamarwa ameendelea kueleza kuwa idadi ya wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma shule ni ndogo zaidi ya wale walio majumbani na ambao hawasomi ingawa wana umri wa kwenda shule, na kuwa majingira mabovu ndicho chanzo cha wanafunzi wengi wenye ulemavu kushindwa kwenda klujiandikisha shule.

Wanafunzi walemavu wa viungo wanapata changamoto hasa nyakati za kwenda chooni ambapo vyoo vimejengwa bila kuzingatia mahitaji yao kwani I nawalazimu kutembea juu ya majo machafu ya chooni kabla ya kufika kwenye shimo la choo.Pia madarasa hayajajengwa kuzingatia mahitaji ya walemavu.

Nchi ina safari ndefu katika kufikia lengo lake la kuwa na elimu inayofikiwa na watoto wote.hii ni changamoto kwa siyo tu mamlaka ya halmashauri ya Musoma bali serikali yote kwa ujumla katika kufikia mahitaji ya kujifunzia/kusomea kwa watoto wa kada zote pasina kujali hali ya mwanafunzi husika mpaka kufikia mwaka 2025.


Picha na Habari na Idara ya habari na Utetezi, HakiElimu
 

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More