Thursday, June 14, 2012

Maisha ya 'geto' ni chanzo cha mimba kwa wanafunzi sekondari ya Iwalanje

Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Iwalanje akijisomea katika moja kati ya chumba cha darasa kilichogeuza bweni shuleni hapo
mmoja kati ya wanafunzi wa shule ya sekondari Iwalanje Mbeya akitoka gheto kuelekea shule

Makamu mkuu wa shule ya sekondari Iwalanje Frank Meck akizungumza na waandishi wa habari waliofika shuleni hapo
Maisha ya geto
WAZAZI wanaosomesha watoto wao katika shule ya sekondari ya Iwalanje kata ya Ijombe wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya wamedai kuwa chanzo cha watoto wa kike kukatisha Masomo kwa mimba limechangiwa uamuzi wa serikali kuwatoa wanafunzi hao katika bweni na kuwaacha kuishi katika katika vyumba vya kupanga maarufu Kama magheto .

Hali hiyo umepelekea baadhi ya wananchi wa kijiji hicho cha Iwalanje kutumia mwanya huo kuwarubuni watoto hao wa kike kwa kuwapangisha nyumba zao na mwisho wa siku wamekuwa wakiwataka kimapenzi na kuwageuza wanafunzi hao ni nyumba ndogo .

Wakizungumza na wanahabari kijijini hapo Jana wazazi hao walisema kuwa pamoja na shule hiyo kuendelea kuwa na sifa nzuri ya kufaulisha ila bado mimba kwa watoto wa kike zimeendelea kuwa ni tatizo .

Anna mwanjala alisema kuwa wananchi wa kata hiyo ya Ijombe walikuwa wamejitolea kujenga bweni kwa ajili ya watoto wa kike Kama njia ya kupunguza tatizo la Mimba kwa watoto hao ila serikali iliamua kuwatoa wanafunzi hao katika bweni lao na kuwaweka watoto wa kiume ambao wanasoma kidato cha Tano na sita.

Alisema kuwa uamuzi huo wa serikali kuifanya shule hiyo kuwa high school na kuwatoa watoto wa kike katika bweni lao na kuwaweka wanafunzi hao wa kiume kutoka nje ya kata hiyo ,wao Kama wazazi na wananchi wa eneo hilo ambao walijitolea kujenga bweni Hilo hawajapendezwa .

Hivyo alisema ili kuondoa masikitiko kwa wananchi waliojenga bweni hilo kwa ajili ya watoto wao wa kike wanaotoka vijiji vya mbali na shule hiyo ni vema serikali kutimiza ahadi yake ya kuwajengea bweni watoto hao wa kidato cha kwanza hadi cha nne ambao wamekuwa wakipata shida kwa kupanga katika magheto mitaani.

"kweli tunashindwa kujua uamuzi wa serikali yetu kuwapokonya bweni watoto wa kike na kuwaweka watoto wa kiume wakati sisi wananchi tulijenga bweni hilo kwa ajili ya watoto wetu wa kike Kama njia ya kupunguza tatizo la mimba"

John Samweli amasema kuwa mbali ya baadhi ya wamiliki wa nyumba kijijini hapo kuwageuza wanafunzi hao kuwa ni wake zao wadogo bado baadhi ya vijana wamekuwa wakiwarubuni wanafunzi hao kwa kuwapa vizawadi vidogo Kama chakula ,mboga na miwa .

Alisema kuwa kutokana na baadhi ya wanafunzi kuishi mbali kijiji hicho wamekuwa wakishindwa kurudi Kwao mwisho wa wiki kwa ajili ya kufuata mahitaji na kutoa nafasi kwa vijana hao kuwasaidia mahitaji hayo kwa sharti la kupewa mapenzi.

Kwani alisema katika kijiji hicho kumekuwepo na matukio ya wanafunzi kukatisha Masomo kwa mimba na kesi zinapopelekwa ofisi za serikali za vijiji na kata wahusika wamekuwa wakiachiwa ama kubadilishiwa mashtaka na kupewa Yale ambayo yanaunafuu wa kupewa dhamana .

Aidha alisema kuwa tatizo la watoto wa kike kukaa nje ya shule ndilo limekuwa likichangia kuwepo kwa mazingira hatarishi ya wanafunzi hao kujisomea.

Makamu mkuu wa shule hiyo Frank Meck alikiri kuwepo kwa tatizo la mimba katika shule hiyo na kuwa chanzo ni jamii inyozunguka shule hiyo kutokuwa na mwamko wa elimu.

Meck alisema kuwa shule hiyo inajumla ya wanafunzi 681 Kati yao wasichana ni 317 na kuwa wanafunzi Wanafunzi wavulana 68 ambao ni Wa kidato cha tano na sita ndio wanakaa katika mabweni Mawili yaliyo shuleni hapo.

Alisema kuwa wanafunzi hao wanaoishi bweni ni wale wanaotoka maeneo ya mbali na kata hiyo huku wanafunzi wasichana 20 Kati ya 68 waliokuwa wakiishia bweni wamekuwa wakilala katika vyumba viwili vya madarasa vilivyogeuzwa Kama mabweni ya muda kwa wanafunzi hao.

Kuhusu tatizo la mimba alisema kuwa Kati ya mwaka 2011 hadi sasa jumla ya wanafunzi 7 wameshindwa kuendelea na msomo kutokana na mimba .

Alisema mwaka 2011 wanafunzi wanne walipata mimba na mwaka 2012 wanafunzi watatu akiwemo mwanafunzi mmoja wa kidato cha nne na wawili kidato cha tatu.

Meck alisema pamoja na kuwa idadi kubwa ya mimba zimesababishwa na jamii inayoizunguka shule hiyo pamoja na wafanyabiashara mmoja Kati ya wanafunzi hao Saba waliokatisha Masomo kwa mimba alipewa mimba hiyo na mwanafunzi mwenzake ambaye walikuwa wamepanga katika getho moja mtaani.

Afisa Elimu sekondari katika wilaya ya Mbeya mwalimu Magreth Mbwilo mbali ya kuthitibidha ukubwa wa tatizo hilo la mimba katika shule hiyo ya Iwalanje bado alisema kuwa katika Wilaya hiyo changamoto kubwa ni mabweni kwa wanafunzi na kuwa kati ya shule 27 za sekondari katika wilaya hiyo ni shule mbili pekee ndizo zinamabweni japo bado hayatoshi.

Alisema mkakati uliopo ni kuendelea kujenga Hosteli zaidi na tayari ujenzi wa Hosteli 10 unaendelea katika shule mbali mbali huku Kati ya Hosteli hizo tatu zipo katika hatua ya mwisho.PICHA NA HABARI NA BLOG YA FRANSIS GODWIN(http://francisgodwin.blogspot.com)
 












0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More