NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO PHILIP MULLUGO.
******
Habari na Joachim Nyambo wa Kalulunga Community Media-Mbarali
Wakazi 18,333 Wilayani
Mbarali mkoani Mbeya hawajui kusoma,kuandika na kuhesabu hali inayozua
changamoto kwa serikali na wadau wengine kuwabadilisha wakazi hao ili
watambue umuhimu wa elimu kwa watoto wao.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Kened Ndingo uwepo
wa idadi kubwa ya wananchi wasiojua kusoma,kuandika na kuhesabu
unachangia kuwepo kwa uelewa duni juu ya umuhimu wa elimu wilayani humo
Ndingo ameyasema hayo katika
kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika katika ukumbi wa kanisa la
Lutherani katika mji mdogo wa Rujewa na kufafanua kuwa pamoja na juhudi
kubwa inayofanywa na serikali kuhakikisha kila mtoto anapata elimu
stahili,uthamani wa elimu kwa wakazi wa wilaya hiyo unaonekana kushuka
siku hadi siku.
Amesema
tofauti na maeneo mengine ambako wakazi wanakimbilia elimu kwa
kuhakikisha waanawawezesha watoto wao kuipata,wakazi wilayani kwake
hawaoni umuhimu huo na imefika waakati sasa hawajali elimu hata kwa
watoto wao.
Kwa
upande wake ofisa elimu shule za msingi Wilayani humo Rustika Turuka
amesema Wilaya imekuwa ikishika kati ya nafasi ya 6 na 8 ya ufaulu
kimkoa kati ya wilaya 8 zilizopo mkoani Mbeya katika matokeo ya darasa
la saba.
Naye mmoja wa wadau waliohudhuria kikao hicho Ophia Nzobonaliba amesema
tatizo kubwa lipo kwa jamii za wafugaji ambao wamekluwa wakiona bora
watoe fidia kwa kutopeleka watoto wao shule na kuwaacha waendelee
kuchunga mifugo yao.
0 comments:
Post a Comment