Thursday, May 31, 2012

Shule za Sekondari wilayani Kilwa mambo safi

Mwanafunzi akifanya mazoezi kwenye kompyuta
Mwanafunzi akiwa anafanya mazoezi kwenye kompyuta
Wanafunzi ndani ya somo la TEHAMA kwa vitendo
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mpunyule wilayani Kilwa wakijifunza somo la TEHAMA kwa vitendo.Shule nyingi nchini zinafundisha somo la TEHAMA kwa nadharia hivyo wanafunzi kubaki na uelewa mdogo wa stadi husika kutokana na kukosa uhalisia wa vifaa vya kufundishia.
 Wanafunzi wa sekondari ya Mpunyule wakiendelea na mazoezi ya Kopyuta.
Huu ni mfano wa kuigwa kwa shule zingine kwani kuwepo kwa mazingira na vifaa vya kufundishia kama vile Kompyuta kunarahisisha uelewa wa wanafunzi. Safi sana shule ya sekondari Mpunyule.

Shule tatu wilayani Kilwa zipo kwenye mpango wa kusaidiwa kompyuta na shirika lisilokuwa la kiserikali la UKENGEE FOUNDATION ambalo toka mwaka 2009, limesaidia zaidi ya wanafunzi 9,000  kusoma  somo la TEHAMA kwa vitendo tofauti na shule zingine za serikali ambao husoma nadharia tuu.

Shule ya Sekondari Mpunyule ni shule ya kata, ina jumla ya kompyuta 20 zinazotumiwa na wanafunzi 264 wa kidato cha kwanza mpaka cha nne.Kutokana na shule kutokuwa na umeme, kompyuta hizi zinatumia umeme wa jua. Shule hii ipo kilometa 105 kutoka kilwa mjini.Hii ni mojawapo ya shule tatu za wilaya ya kilwa zenye vifaa hivi adimu kwa shule nyingi nchini. Shule zingine zenye kompyuta wilayani Kilwa ni Kilwa Day na Ilulu.
Picha zote na Edwin Mashasi aliyekuwa Kilwa.

2 comments:

Hongera sana uongozi na wote waliofanikisha hilo

halafu ooh miaka hamsini hakuna kilichofanyika...jamani !

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More