Tuesday, May 22, 2012

Mazingira ya kujifunzia ni chanzo cha utoro wa wanafunzi walemavu Namtumbo


Wanafunzi walemavu wa Hakili shule ya msingi Namtumbo wakiwa ofisi ya walimu.Wanafunzi hawa hawana darasa maalumu la kusomea kwani wakati mwingine huchuliwa na mwalimu wao na kuwapeleka nyumbani kwake ili kuwapatia chai na kuwafundishia nyumbani kwake. Ukosefu wa chakula na madarasa ya kusomea kwa wanafunzi walemavu umesababisha wanafunzi hawa kuwa na mahudhurio madogo na wengine kutokuhudhuria kabuisa.

Mwalimu wa kietngo maalumu cha shule ya msingi Namtumbo Bw Lezile Kampango amesema changamoto kubwa katika kituo hicho pekee cha wanafunzi wenye ulemavu wa hakili wilayani namtumbo ni ukosefu wa chakula,vifaa vya kufundishia, madarasa na walimu.



“Watoto kama hawa hawawezi kusoma bila chakula, kwani mwanafunzi akihisi njaa tu anatoka nje na kurudi kwao bila hata ya kuuliza, gari ikipita wote wanatoka na kulikimbilia, ukiwa mwalimu inabidi uhakikishe kuna vivutio vya kutosha kuwafanya wafike shule na kukaa madarasani,” alisema Kampango.




Wilaya ya namtumbo ina kitengo kimoja tu cha watoto wenye mahitaji maalumu kilichopo katika shule ya msingi Namtumbo kinachohudumia wanafunzi wenye ulemavu wa hakili tu.Kitengo hiki kina mwalimu mmoja na wanafunzi watano wanaohudhuria kati ya 26 walioandikishwa.
Kitengo hicho akilianzishwa mwaka 1997 na ndicho kitengo pekee kinachoshughulia kutoa elimu kwa watoto wenye ulemavu katika wilaya nzima ya Namtumbo kwa kuwa hakuna kitengo wala shule ambayo inatoa elimu maalum katika makundi mengine ya wenye ulemavu kama wasioona na viziwi.




 Takwimu za mwaka 2011za zinaonesha kuwa, wilaya ya Namtumbo ina jumla ya walemavu 252, kati yao wanafunzi 181 ndio wanaosoma shule mbalimbali katika elimu jumuishi wakiwemo wenye ulemavu wa akiri 34,wasioona 18,viziwi 11,walemavu wa viungo 109 na albino tisa.
Wanafunzi 71 waliokuwa na umri wa kwenda shule hawajaandikishwa na hawapo mashuleni wakiwemo wenye ulemavu wa akiri 21,wasioona mmoja,viziwi 11,wenye ulemavu wa viungo 35 na albino watatu. 







Takwimu za shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto ulimwenguni(UNICEF) za mwaka 2002 zilionesha kuwa asilimia 98 ya watoto wenye ulemavu katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania hawapatiwi kabisa elimu jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wao.
Imeelezwa kuwa asilimia hii ndogo inasababishwa na kuwepo kwa shule chache maalum hapa nchini kwa ajili ya watu wenye ulemavu,ukosefu wa wataalamu,sera na sheria nyingi za nchi hizo  hazitaji moja kwa moja au kutoa utaratibu mzuri wa kutoa elimu kuhusu wenye ulemavu,ukosefu wa vifaa maalum na muhimu vya kuwawezesha kusoma pamoja na miundo mbinu duni  isiyokidhi mahitaji  ya watu wenye ulemavu.



0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More