Thursday, March 22, 2012

Lowassa Akuatana na Walimu wa Shule ya Sekondari ya Engutoto kujadili sababu za kufanya vibaya kwenye mtihani wa Taifa





Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza kwa kusisitiza wakati wa mkutano wake na Walimu wa Shule ya Sekondari ya Engutoto,Wilayani Monduli kuhusiana na hali ya elimu katika shule hiyo kutoridhisha na kupelekea wanafunzi wengi wa shule hiyo kufeli kwenye mtihani wa taifa wa kidato cha nne.Mkutano huo umefanyika leo shuleni hapo,ambapo walimu wa shule hiyo walitoa changamoto mbali mbali wanazomabiliana nazo.Mh. Lowassa amewaasa walimu wa Shule hiyo kuwa wafanye kazi kwa juhudi ili kuwaandaa vijana wa taifa la baadae.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo,Bw. Joseph Lukumay.

Walimu wa Shule ya Engutoto iliyopo Wilayani Monduli Mkoani Arusha,wakizungumzia changamoto mbali mbali wanazokabiliana nazo katika kazi yao ambapo wengi wamedai kuwa inachangia kwa kiasi fulani kudhorota kwa elimu katika shule hiyo.





Afisa Elimu Wilaya ya Monduli,Bw. Shaaban Mngunye (kushoto) akifafanua jambo wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunde wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa kabla ya kuanza kwa mkutano na Walimu wa Shule ya Sekondari ya Engutoto iliyopo Wilayani humo.


Afisa Elimu Wilaya ya Monduli,Bw. Shaaban Mngunye (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (wa pili kulia) wakati wa mkutano na Walimu wa Shule ya Sekondari ya Engutoto,Wilayani Monduli.Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo,Mwl. Ally Muyago na wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo,Bw. Joseph Lukumay.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Shule ya Sekondari ya Engutoto,Bw. Joseph Lukumay akitoa maelezo mafupi na kuwataka walimu wa shule hiyo kuanza kuzungumzia ni kwanini shule yao imefanya vibaya kwenye mtihani wa taifa wa kidato cha nne.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimsikiliza kwa makini,Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Shule ya Sekondari ya Engutoto,Bw. Joseph Lukumay.


Picha na habari na Blog ya HakiNgowi

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More