Wednesday, February 8, 2012

Wanaharakati Dar wafunga barabara wakidai huduma za afya kurudishwa mahospitaliniBwana Irinei Kiria akimueleza askari wa barabarani wa kituo cha daraja la salenda juu ya nia ya mtandao wa wanaharakati kufunga barabara ili kuishinikiza serikali kumaliza tofauti zake na madaktari ili kurudisha huduma za afya mahispitalini.

Madaktari kwa zaidi ya wiki moja sasa wamekuwa katika msuguano na serikali na hivyo kuamua kugoma na kusababisha kuzorota kwa huduma za afya katika hospitali za srikali ikiwemo hospitali ya Taifa ya Muhimbili.


Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu Bi Helen Kijo-Bisimba akiwa na bango lenye ujumbe kwa serikali ukimtaka rais Jakaya Kikwete kuwafuta kazi mara moja Waziri wa Afya na ustawi wa jamii Dr Haji Mponda, Naibu waziri wake Dr Lucy Nkya, katibu mkuu Blandina Nyoni na Mganga mkuu Dr Deo Mutasiwa kwa kushindwa kuzuia mgomo wa madaktari nchini.Aliyekaa katikati ni mkurugenzi wa Tamwa Ananilea Nkya na kushoto ni Anastazia Rugaba wa HakiElimuMabango zaidi0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More