Saturday, November 26, 2011

Sababu za shule maalumu za serikali kushuka kiwango cha ufaulu zatajwa


Kaimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Msalato,Dodoma Mwl Chrisant A. Makwaya

Baadhi ya sababu kuu zilizopelekea shule zilizokuwa za vipaji maalumu kama shule ya Msalato kushuka viwango vya ufaulu kwenye mitihani ya taifa.

sababu hizo ni ruzuku kutofika kwa wakati na zikiwa pungufu na malengo yaliyokusudiwa, mfano ruzuku kama imepangwa shilingi elfu 25 kwa mwaka kwa kila mwanafunzi, ikaja shilingi elfu 12 tuu na ikiwa imechelewa ni ukweli zitaathiri utendaji kazi wa walimu na usomaji wa wanafunzi.

Maslahi duni kwa walimu ni chanzo cha kushuka kwa utendaji kazi wa walimu na uwajibikaji.


Meza kuu katika kongamano la miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara, tathmini ya hali ya elimu nchini, wakiongozwa na mwenyekiti wa kongamano Mwl Ayub Rioba kutoka Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.Wengine ni Prof Herme Mosha na Dr Kitila Mkumbo wote wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam



Washiriki wa kongamano wakichangia hoja mbalimbali za elimu ambazo kwa kiasi kikubwa zilikua zinatoa mwelekeo wa nini cha kufanya ili kuboresha elimu nchini.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More