Tuesday, November 1, 2011

Picha na Matukio siku ya kufungua maktaba ya kisasa

wanafunzi wa shule ya msingi Mwisenge wakiimba shairi maalum kwa mgeni rasmi ambaye ni Capt Geofrey Ngatuni mkuu wa wilaya ya Musoma na wageni kutoka HakiElimu siku ya kufungua rasmi maktaba iliyojengwa na HakiElimu katika kumuenzi baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere
Mkurugenzi wa HakiElimu Elizabeth Missokia akitoa machache juu ya umuhimu wa maktaba katika utoaji wa elimu bora.Pembeni kushoto ni Capt Geofrey Ngatuni mkuu wa wilaya ya Musoma


wafanyakazi wa HakiElimu na walimu wa shule ya msingi Mwisenge wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi mbele ya maktaba iliyofunguliwa rasmi.Maktaba hii imejengwa na HakiElimu

Wanafunzi wakiwasikiliza wageni wao kwa makini

Mtaalam wa masuala ya maktaba kutoka HakiElimu Bi Agnes Mangweha (Kushoto) akiwa na Meneja wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu Glory Mosha.

Burudani nazo zilitawala huku wanafunzi wakiwa na shauku ya kuhakikisha wageni wao wanaburudika.

1 comments:

jamani kwa kweli hiki ni kitu cha msingi sana hasa kwa wanaharakati , ninaamini hii itakuwa nichangamoto kwa shule zote ambazo hazina maktaba kujitahidi kuipztz ili wanafunzi wapate wanachotakiwa kukipata

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More