Thursday, November 3, 2011

Mama Maria Nyerere: HakiElimu kazi yenu ina tija kubwa kwa Taifa


Mkurugenzi wa HakiElimu Elizabeth Missokia akikabidhi zawadi kwa mke wa baba wa Taifa Mama Maria Nyerere nyumbani kwake Mwitongo- Butiama.HakiElimu ilifanya ziara hiyo nyumbani kwa baba wa Taifa na rais wa kwanza wa Tanzania Mwl Julius Nyerere.Katika kutambua mchango wa mwalimu katika sekta ya elimu, HakiElimu ilimzawadia mama Nyerere vitu mbalimbali ikiwemo picha na nakala ya vitabu vya Mwl Nyerere hiyo yote ni katika kutambua mchango wake katika kumsaidia Mwl katika shughuli zake


Hapo Mama Nyerere akikabidhiwa zawadi ya picha yenye maneno ya shukrani


Mkurugenzi wa HakiElimu akiteta jambo na familia ya Mwl Nyerere, ambao ni Bi Rosemary Nyerere mtoto wa Mwl Nyerere na mama Maria Nyerere.


Taswira za matukio ya wafanyakazi wa HakiElimu Nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwl Nyerere Mwintongo - Butiama

Daniel Luhamo,Meneja katika idara ya fedha -HakiElimu nae alipata fulsa ya kupata kumbukumbu ya picha na mama Maria Nyerere


Kwa pamoja, tunakushukuru mama

Watoto wa hayati Mwalimu Nyerere, Bi Rosemary na Madaraka Nyerere nao walikuwepo


Wana familia ya HakiElimu wakiwa nyumbani kwa Mama Maria Nyerere








0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More