Saturday, November 26, 2011

Katiba mpya itatue changamoto za viziwi katika kupata elimu



Mtaalam wa lugha za alama akiwafafanulia baadhi ya washiriki wa kongamano wenye changamoto za kusikia (Viziwi).

Watu wenye changamoto ya kusikia wameiomba serikali kuweka mikakati mbadala ili kuweza kuzalisha walimu na wataalam wa lugha za alama ili kuwawezesha kuwa na mazingira mazuri katika kupata elimu kama wengine.
"Mfano wenzetu wanaosikia wana uwezo mkubwa wa kusoma na kuandika tofauti na viziwi.kwa sasa hivi mfumo mzima wa elimu haujawawezesha walemavu hasa viziwi.viziwi wanatumia miaka 10 ili kumaliza darasa la saba tofauti na wenzetu wanaosikia ambao huchukua miaka saba tuu kumaliza." mmoja wa watu wenye changamoto za kusikia alisikika kwenye kongamano la elimu.
Viziwi wengi wanaishia kutokumaliza elimu yao ya msingi na hata wachache wanaojiandikisha sekondari, wachache sana ndio wanafika elimu ya juu mara nyingi mtu mmoja au wawili tuu kwa mwaka na hata miaka mingine hakuna anaefika ngazi hiyo.
wasiosikia hao wameomba kujumuishwa katika katiba mpya na kuelezwa jinsi serikali itakavyoweza kushughulikia changamoto za walemavu viziwi.
Baadhi ya waliohuzulia kongamano wenye changamoto za kusikia (Viziwi)


Hawa ni washiriki wenye uwezo wa kusikia.Je tofauti zao zinaonekana kiurahisi?

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More