Tuesday, November 1, 2011

HakiElimu yajenga maktaba ya kisasa kumuenzi baba wa Taifa

Mkurugenzi wa HakiElimu Elizabeth Missokia akiwa mbele ya jengo la maktaba lililojengwa na HakiElimu katika shule ya msingi Mwisenge ambako Mwl Nyerere alisoma enzi hizo


Mkuu wa wilaya ya Musoma Capt Geofrey Ngatuni aliyemwakilisha mkuu wa mkoa Bw John Tupa akipata maelezo kutoka kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mwisenge katika ufunguzi wa Maktaba ya mfano ambayo imejengwa na HakiElimu katika kutambua mchango wa muasisi wa Taifa la Tanzania katika Elimu.

Wafanyakazi wa HakiElimu wakiwa mbele ya Maktaba hiyo mpya, kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa HakiElimu Elizabeth Missokia, Meneja wa idara ya ushiriki wa wananchi Pius Makomelelo, Afisa katika idara ya utawala Fredrick Rwehumbiza na Meneja wa idara ya utawala na rasilimali watu Bi Glory Mosha.

Nukuu mojawapo ambayo iliwahi kutolewa na Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere. Nukuu hii ilichaguliwa kutoa hamasa ya wanafunzi kupenda kusoma vitabu katika maktaba mpya ya shule ya msingi Mwisenge.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More