Tuesday, November 22, 2011

Kongamano la elimu kufanyika UDSM jumamosi hii


Tumejaribu, tumeweza kiasi, tunahitaji kufanya zaidi ili kusonga mbele.

HakiElimu kwa kushirikiana na Umoja wa walimu wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wameandaa kongamano kubwa kuwahi kutokea nchini lenye lengo la kutathmini hali ya elimu nchini; miaka 50 tangu Tanzania bara kupata uhuru wake mwaka 1961.

Tumetoka wapi, tupo wapi na wapi tunaelekea:hapa tulipo tunaridhika napo?nini kifanyike ili kuboresha zaidi hali hii?tunajifunza nini katika miaka hii 50?tunajivunia nini na elimu yetu imetoa mchango gani katika taifa? sekta hii inathaminiwa?hayo ni baadhi tu ya maswali ambayo majibu yake yatakuwa wazi jumamosi hii katika ukumbi wa Yombo 4 Udsm.

Wazungumzaji wakuu ni Waziri wa Elimu wa Serikali ya Awamu ya Kwanza Mh Jackson Makweta na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof Justinian Galabawa.

Karibuni nyote


0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More