Wednesday, September 28, 2011

Wanaharakati waongelea siku ya haki ya kupata taarifa

Dr Sengondo Mvungi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam akichangia mada ya umuhimu wa sheria ya habari na haki ya mtanzania kupata, kupewa na kutafuta habari.Mjadala huu ulirushwa moja kwa moja na kituo cha redio cha Wapo FM, ambapo matangazo yalirushwa kutokea ofisi za HakiElimu.


Mdahalo huo umefanyika leo ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya wiki ya haki ya kupata taarifa duniani.Tangu mwaka 2007, wadau wa habari na watanzania kwa ujumla wamekua wakidai kuwepo kwa sheria ya habari (Right to information law), lakini hadi sasa imekua kitendawili.

Mwandishi na mtangazaji wa kituo cha redio cha Wapo FM akiongoza mjadala huo

Mafundi mitambo nao walikuwepo kuhakikisha matangazo yanaruka bila mtafaruku wowote1 comments:

waandishi wamelala sana katika kutetea hili wakati hili ni kwa manufaa yao wenyewewaandishi wamelala sana katika kutetea hili wakati hili ni kwa manufaa yao wenyewe

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More