Monday, September 5, 2011

Wanafunzi Milioni Moja kuanza mtihani wa Darasa la Saba Kesho

Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo

Serikali imetangaza rasmi mtihani wa darasa la saba kuwa utafanyika kesho Tarehe 7 na 8/09/2011 nchini kote huku zaidi ya wanafunzi Milioni Moja wakiwa tayari kuanza mtihani huo.

Mwaka huu, watahiniwa wa kike ni wengi zaidi ya wenzao wa kiume hali inayoashiria kua fursa za elimu kwa mtoto wa kike zinaongezeka tofauti na miaka ya nyuma.

Kwa mwaka huu watahiniwa wapatao 1,010,619 watafanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.

Hayo yamo kwenye taarifa iliyotolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo.
Kati ya watahiniwa wote wasichana ni 527,125 sawa na asilimia 52.15% na wavulana 483,494 sawa 47.84% ya watahiniwa wote.

kati ya watahiniwa wote, 993,327 watafanya mtihani kwa lugha ya kiswahili na watahiniwa 17,295 wanatarajiwa kufanya mtihani huo kwa lugha ya kiingereza.

Watahiniwa wasioona wanaotarajiwa kufanya mtihani ni 96.


0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More