Tuesday, September 20, 2011

Shule za Kata:Ghala linapogeuzwa bweni la wanafunzi

Hili ndilo ghala la kuhifandhia nafaka lililopo karibu na shule ya sekondari Mbabala. Ghala hili limebadilishwa matumizi na kuwa bweni la kulala wanafunzi (wavulana) wapatao 43 huku kukiwa bila matengenezo yoyote.


Muonekano wa bweni hilo kwa ndani
Na hiki ndicho choo wanachotumia wanafunzi takriban 43 wa bweni hilo

walioshindwa kupata nafasi kwenye bweni hilo kwa sababu mbalimbali wameamua kupanga mageto mitaani.

Huyu ni mmojawapo wa wanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Mbabala ambaye pia ni mmojawapo wa waliopanga mageto mitaani ambaye anakerwa na maisha ya kupanga mageto kwani kunamsababishia kupoteza muda mwingi katika utafutaji wa maji, kupika na pia kazi nyingine za nyumbani.

Picha kwa hisani ya blog ya mtandao wa elimu, Dodoma.

Hongereni sana wana mtandao huu wa pale Dodoma.mchango wenu katika sekta ya elimu unaonekana. msikate tamaa na endeleeni kutupasha habari sisi wote hasa tunaotembelea blog ya HakiElimu.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More