Monday, September 26, 2011

Kawambwa: Tumedhibiti udanganyifu na uvujaji wa mitihani

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Dr Shukuru Kawambwa, amewahakikishia watanzania kuwa mitihani ya kidato cha nne haitavuja hivyo kuwataka wanafunzi kujiandaa kikamilifu ili kufanya mitihani kwa juhudi za darasani na si vinginevyo katika mitihani ya kidato cha nne inayoanza wiki ijayo.


Mheshimiwa kawambwa aliyasema hayo katika mahafali ya kidato cha nne ya shule ya sekondari Jitegemee ya jijini Dar es Salaam, shule ambayo inamilikiwa na jeshi la kujenga taifa (JKT).

Kawambwa pia aliwataka wanafunzi kuepuka udanganyifu wa aina yoyote katika mitihani ijayo huku akisifu juhudi za serikali katika kuongeza ufaulu na wengi kujiunga na kidato cha tano.

"Nawaomba wazazi kuacha tabia ya kuwatafutia wanafunzi mitihani ya wizi kwani kufanya hivyo ni kuwadumaza watoto akili zao ambazo walimu wamezitayarisha kwa miaka minne na hivyo kuwa chanzo cha wanafunzi hao kufeli na hivyo kuwavurugia maisha yao kutokana na mipango ya kuhakikisha mtihani hauvuji." alisema Dr Kawambwa.

Dr kawambwa akiwatunuku wanafunzi wa shule ya sekondari Jitegemee vyeti vya kumaliza kidato cha nne siku ya jumamosi iliyopita.

Dr Kawambwa akiondoka eneo la sherehe ambapo alikua mgeni rasmi.Pembeni ni mkuu wa shule ya sekondari Jitegemee Meja Martine Mkisi


Picha na matukio na Vicent Manyanyika

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More