Tuesday, September 20, 2011

Biashara ya vyuma chakavu zinavyo athiri maendeleo ya wanafunzi mjini Dodoma

Biashara za vyuma chakavu ni moja ya biashara ambazo zimeteka sana muda wa watoto mkoani Dodoma kwani hutumia muda mwingi kuzagaa mitaani na kutafuta vipande vya chuma kwaajili ya kwenda kuuza.Mtoto huyu mwenye umri wa kwenda shule alikutwa akitafuta vyuma chakavu kwa kwenda kuviuza.


Kijana huyu ni mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi mnadani akiokota vyuma chakavu kwaajili ya kuviuza.Anadai kuwa hufanya kazi hii nyakati za mwishoni mwa juma, siku za sikukuu na likizo ili kujipatia fedha kidogo zitakazomsaidia kununua vitu muhimu kama madaftari na peni kwaajili ya shule.

Samsoni mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Ngh'ongh'onha manispaa ya Dodoma akiwa amebeba miwa kwaajili ya kuuza.

Picha kwa hisani ya Blog ya marafiki wa Elimu Dodoma

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More