Thursday, August 25, 2011

TGNP WAMILIKI HALALI WA JENGO LILILOPO MABIBO DAR ES SALAAM


Mtandao wa jinsia tanzania ni wamiliki halali wa jengo lenye hati namba 56998,kiwanja namba 22/3/1 lililopo Mabibo Dar es Salaam.

TGNP walinunua jengo hilo kutoka mufilisi benki ya rasilimali Tanzania (TIB) kwa iliyokua Tanzania sewing thread manufacturers limited ambayo ilikua kamouni tanzu ya Tanzania textile company limited (Texco) kwa gharama ya shilingi Milioni 200 ambapo makubaliano ya manunuzi yalifanyika tarehe 15 June 1997.

Mchakato wa uuzaji wa jengo hili ulikua wa wazi ulitangazwa katika vyombo vya habari hususani Magazeti.

Baadhi ya watumiaji wa ofisi walikua ndani ya jengo hili wakati Texco ilikua inafirisiwa nao walishiriki katika mchakato wa kununua bila mafanikio.Baada ya TGNP kushinda tender,baadhi ya watumiaji hao mnamo mwezi wa July 1997, walifungua kesi namba 215/1997 dhidi ya TIB mshitakiwa wa kwanza na TGNP mshitakiwa wa pilikatika mahakama kuu kupinga maamuzi ya TIB kuiuzia TGNP jengo hilo.

UAMUZI WA MAHAKAMA KUU

kesi hii ilichukua muda mrefu sana takribani miaka 12 mpaka kufikia tarehe 19/9/2009, uamuzi wa mahakama kuu ulipotolewa na mheshimiwa jaji T.B Mihayo wa mahakama kuu hukumu ambayo iliwapa haki TGNP na kuwaamuru walalamikaji kuondoka mara moja na kulipa gharama.

wakati mchakato wa kutekeleza hukumu ya mahakama kuu ukiendelea, mnamo tarehe 19/9/2009 walalamikaji walipeleka katika mahakama ya rufaa azimio la kusimamisha utekelezaji wa hukumu ya mahakama kuu wa kutowatoa kwenye jengo na kupitia ombi namba 129 la 2009 ombi lao limetupiliwa mbali na mahakama ya rufaa tarehe 23/8/2011.

MCHAKATO WA KUTEKELEZA UAMUZI WA MAHAKAMA

TGNP wamiliki halali wa jengo hili tunasubiri utekelezaji wa uamuzi wa mahakama ya rufaa iliyotolewa tarehe 23/9/2011.Tutaendelea kuwataarifu maendeleo ya mchakato huu.

Usu Mallya, Diana Mwiru

Mkurugenzi mtendaji, Mkuu wa chuo cha mafunzo ya jinsia (TGI)

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More