Tuesday, July 19, 2011

Serikali kutoa mafunzo ya walimu 2,052 wakiwa kaziniWaziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dr Shukuru Kawambwa leo amesoma bajeti ya elimu kwa mwaka wa fedha 2011/2012, katika bajeti hiyo, jumla ya Sh Bilioni 659.298 zimetengwa kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya wizara.

Katika mwaka wa fedha 2011/2012, serikali itaendesha mafunzo kazini kwaajili ya walimu 2052 wanaofundisha masomo ya sayansi,hisabati na lugha kwa shule za msingi na sekondari nchi nzima ili kuinua kiwango cha ufundishaji kwa masomo hayo.

Pia serikali imeongeza fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka Sh5,000/- mpaka 7,500/- kwa siku.

Uchambuzi zaidi utawajia kesho.


0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More