Friday, June 10, 2011

HakiElimu yawaaga wafanyakazi wa shirika la Muhuri


Rahma na Asha wafanyakazi wa shirika lisilo la kiserikali la Muslim for Human Rights (Muhuri) la Mombasa Kenya wakiwapungia mkono wa kwa heri wafanyakazi wa HakiElimu katika Hafla ya Chakula cha mchana kilichoandaliwa maalum kwa kuwaaga. Hafla hiyo ilifanyika leo katika ukumbi wa harakati summit ndani ya jengo la ofisi za HakiElimu lililopo Upanga jijini Dar es Salaam.


"Nawashukuru sana kwa ukarimu wenu mliotuonesha kwa kipindi chote tulichokuwa hapa, kweli tumefaidika sana na tuliyojifunza, ati wenzetu mpo mbele sana," alisema Bi Asha wakati akitoa pongezi zake kwa shirika la HakiElimu kwa kuwapokea na kuwaonesha upendo pamoja na kazi kwa kipindi chote cha siku nne.

Wafanyakazi wa HakiElimu hawakuwa nyuma, baada ya chakula cha mchana walikaa kwa picha ya Pamoja.


Sisi ni familia Moja, tuite Familia ya 'HakiElimu.'Picha zote na Edwin Mashasi

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More