Thursday, June 9, 2011

Bajeti ya serikali ya 2011/2012 haijafikia malengo ya Mkukuta na Millenia

Waziri wa Fedha na Uchumi Mustafa Mkulo akionesha mkoba wenye nyaraka za bajeti ya mwaka 2011/2012.Picha kwa hisani ya Bunge

Kwa miaka minne iliyopita Bajeti ya sekta ya elimu imekua kama gari linalosafiri ambalo lilianza na mwendo mkali lakini mwendo wake unapungua kila baada ya muda.Mwaka wa fedha wa 2008/2009 bajeti ya sekta ya elimu iliongezeka kwa asilimia 32 (ongezeko la bilioni 344).Mwaka huu bajeti ya elimu imeongezeka kwa asilimia 12 tu tofauti na sekta zingine kama miundombinu.

Pia mwaka 2008/2009 ndo mwaka pekee ambo bajeti ya sekta ya elimu ilifikia lengo la Mkukuta na Millenia ambapo bajeti ya sekta ya elimu ilifikia asilimia 20,lakini kuanzia mwaka wa fedha 2009/2010 imekua ikipungua kila mwaka hadi kufikia asilimia 17 ya bajeti ya Taifa.

ufuatao ni mchanganuo wa bajeti ya elimu kila mwaka

Mwaka Bajeti ya Elimu Ongezeko na asilimia uwiano wa bajeti ya elimu na taifa
2008/2009 1.430 Trilioni 344 Bilioni (32%) 20%

2009/2010 1.743 Trilioni 313 Bilioni (22%) 18%

2010/2011 2.045 Trilioni 302 Bilioni (17) 18%

2011/2012 2.283 Trilioni 238 Bilioni (12) 17%

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More