Friday, March 25, 2011

Matokeo ya utafiti wa ruzuku kwa shule za sekondari

1. Asilimia 93 ya shule zilizofanyiwa utafiti zilikua hazijapata fedha za ruzuku kutoka serikalini mpaka kufikia tarehe 31 mwezi wa kwanza 2011.

2. Shule chache zilizopata ruzuku kutoka serikalini, zilipata wastani wa Sh 517/- kwa kila mwanafunzi badala ya Sh10,000/-ambazo serikali ilipanga kutoa.

3. Ruzuku zilizotolewa mwezi wa kwanza 2011 kutoka hazina kwendakwenye halmashauri na kupelekwa kwenye shule za sekondari zilikuwa ni wastani wa Sh390 kwa mwanafunzi mmoja.

4. kati ya mwezi wa sita mpaka mwezi wa kumi na mbili, shule zilipata wastani wa Sh2,087 kwa mwanafunzi.

5. kuna ushahidi mdogo kuwa mfumo wa elimu umejiandaa vya kutosha kuhakikisha upelekaji wa ruzuku mashuleni unafanyika kwa uhakika tena kwa muda uliopangwa na ufuatiliaji makini wa rasilimali zitokanazo na ruzuku mashuleni kitu kinachokwamisha juhudi za kuboresha elimu.

6. Mamlaka husika zinatakiwa kuangalia kwa nini haya yanatokea na kuingilia kati haraka iwezekanavyo na kuwa na uwazi katika uhamishaji wa ruzuku kwenda ngazi ya halmashauri.

0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More