Monday, March 21, 2011

Katiba ni Muhimu sana kwa vijana.



'Lazima niielewe katiba ya sasa ndipo nichangie kuhusu katiba mpya'.mwananfunzi wa shule ya msingi ambaye alikua mmoja wa washiriki waliojumuika katika kongamano la vijana lililofanyika katika viwanja vya HakiElimu mapema mwezi huu.Wengi wa wanafunzi walionesha hamu ya kuijua katiba ya nchi baada ya kuibuka mijadala mingi ya kitaifa dhidi ya katiba iliyopo sasa na kudai kuandikwa kwa katiba mpya.

mjumuiko wa vijana ulikua ni mwendelezo wa maadhimisho ya miaka 10 ya shirika la HakiElimu ambalo kwa maoni ya wadau wengi limefanya kazi kubwa sana kwa kushirikiana na jamii kukuza uelewa juu ya masuala nyeti ya elimu nchini na hivyo kuchochea mijadala chanya juu ya mfumo wa elimu nchini.


Ngoja nisome katiba kwa makini sasa........

Azimio la Arusha lisisahaulike kwenye katiba mpya


Katiba isiache nyuma masuala ya elimu na Haki ya mtanzania kupata elimu...



wanafunzi wanaendelea na maoni yao juu ya kijana na maadili,kijana na elimu pamoja na maoni yao kuhusu kuhusishwa kwao kwenye uandikwaji wa katiba mpya.


0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More