|
Mkurugenzi wa HakiElimu Elizabeth Missokia atoa tamko siku ya uzinduzi wa kampeni ya kuboresha elimu ya awali.Pembeni ni Mratibu wa shirika la Tahea kutoka Mwanza Bi Mary Kabati. |
Leo tarehe 27 Septemba 2012, shirika la HakiElimu linazindua kampeni ambayo imepewa
jina la “Boresha Elimu ya Chekechea”.
Lengo la kampeni hii ni kuitaka Serikali itimize ahadi na wajibu wake wa kutoa
elimu bora kwa wanafunzi wote wa elimu ya awali) ambayo ni muhimu sana katika
kujenga msingi imara kielimu. Ni ukweli usiopingika kuwaelimu ya awali itolewapo kikamilifu, huwa ni msingi imara kwa mtoto katika elimu yake ya baadae.
Elimu
ya Awali ni muhimu kwa maendeleo ya mtoto kimwili, kiakili na kimaadili. Katika
Sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 1995 Serikali inaonesha umuhimu wa elimu ya
awali,inapotamka ; “Tafiti kadhaa zilizofanyika
nchini katika miaka ya 1980 zilibaini kuwa watoto waliopitia elimu ya awali
huwa na mafanikio makubwa zaidi wanapoanza darasa la kwanza. Kutokana na
kutambua umuhimu huu, Serikali iliamua kuingiza Elimu ya Awali kwa watoto wenye
umri wa miaka 5 na 6 kwenye mfumo rasmi wa elimu na kila shule ya msingi
inapaswa kuwa na madarasa ya Elimu ya Awali.”
Sera ya Elimu na Mafunzo 2010. Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi . Toleo jipya Rasimu ya 2 March 2011.(uk 5-6).
Uwekezaji katika huduma bora kwa
mtoto na elimu ya awali huwa na faida maradufu kwa watoto wetu- ambao ni raia wetu wa baadaye. Walipa kodi nao pia hufaidika na
huimarisha uchumi. Faida ya uwekezaji wa fedha za umma katika elimu bora ya
awali ni kubwa sana. Lakini je, Tanzania imeligundua hili na
kulitekelezakikamilifu? Na je, maneno
haya ambayo sera inasisitiza yako yanatekelezwa kwa vitendo?
Baada ya kufanya tafiti
katika sehemu mbalimbali nchini
HakiElimu inasikitishwa na jinsi ambavyo elimu ya awali inavyotolewa
katika mazingira yasiyofaa hali inayochangia kushuka kwa kiwango cha elimu
nchini. Kama ilivyo katika elimu ya msingi
na ile ya sekondari , elimu ya awali imegubikwa na changamoto nyingi. Baadhi ya
changamoto hizi ni upungufu mkubwa wa
vyumba vya madarasa, unaosababisha mrundikano mkubwa katika madarasa, ukosefu mkubwa wa walimu wenye taaluma ya elimu
ya awali pamoja na vifaa vya kufundishia. Aidha, kutokuwepo na tofauti ya
kimadarasa katika elimu ya awali ( yaani watoto wa umri wa miaka 5 na miaka 6
kusoma katika darasa moja), na wingi wa masomo pia ni changamoto.
|
Baadhi ya wanafunzi wa awali kutoka shule ya msingi Mchangani kutoka Mwananyamala Dar es Salaam |
Akiwasilisha Bungeni
makadirio na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2012/2013, Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi , Dkt Shukuru
Kawambwa, alisema Serikali ilitoa mwongozo unaoelekeza kila shule ya Msingi
kufanya Serikali imeelekeza yafuatayo
katika sekta ya elimu nchini kuhusiana na Elimu ya Awali:
(i)
Kuhakisha
kuwa kila shule ya msingi ina darasa la Elimu ya Awali, lenye madawati
yanayolingana na hali ya watoto wa elimu hiyo,
(ii)
Kujenga
vyoo kwa ajili ya watoto wa Elimu ya Awali wasiingiliane na wale wa shule za
msingi.
(iii)
Kuandaa
waalimu wengi wa Elimu ya Awali na kuwapanga katika shule zinazohusika
Katika kutekeleza
maagizo hayo Serikali ilitoa mwongozo
unaoelekeza kila shule ya msingi kuwa na darasa la Elimu ya Awali. Pia wizara
iliahidi kushirikiana na Halmashauri ili kuhakikisha kuwa Elimu ya Awali
inapata rasilimali stahiki kama inavyoelekezwa katika MMEM II, ikiwa ni pamoja
na upatikanaji wa walimu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
Lakini licha ya agizo
hilo pamoja na makubaliano mengine yaliyofikiwa na serikali katika mwaka wa fedha
2012/2013, Serikali haijatenga kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya elimu ya Awali.
Hili linatupa wasiwasi wadau wa elimu kama kweli Serikali ina nia ya dhati kuboresha elimu ya awali nchini au bado inaendelea
kuja na mikakati ambayo haina utekelezaji.
Baada ya kuona madhara ya
kukosa elimu bora ya awali kwa watoto wetu, HakiElimu inatoa wito kwa
watanzania wote nchini wenye mapenzi mema na maendeleo ya taifa letu kuungana
nasi katika kampeni hii kwa njia zifuatazo;
- Kuhimiza
wananchi wote wenye watoto wenye umri wa kuandikishwa shule za awali wafanye
hivyo kwa wingi. Kuna baadhi ya sehemu inaripotiwa wazazi bado hawajaelewa
umuhimu wa kuwapeleka watoto katika madarasa haya ya awali.
- Kuwabana viongozi wetu tuliowachagua
kuanzia mwenyekiti wa mtaa, diwani na Wabunge wetuwanachukua hatua kukabiliana
na changamoto zilizopo ili kufanikisha Elimu bora ya Awali kwa watoto
wetu.
- Wananchi
kuandika barua kwenye magazeti mbalimbali hapa nchini zikielezea hali ya
elimu ya awali inavyotolewa katika maeneo mliyopo. Barua hizo mnaweza
kuzituma moja kwa moja kwenda kwa Wahariri wa magazeti mnayoyasoma kupitia anuani zilizopo
katika gazeti ulipendalo. Vilevile mnaweza kututumia barua hizo kupitia
sanduku letu la barua 79401 DSM; zikiwa na kichwa cha habari ‘BORESHA CHEKECHEA’.
Sisi tutazipeleka katika magazeti mbalimbali nchini na zitachapishwa na
kufikisha ujumbe kwa viongozi wetu.
- Aidha,
ili kuchagiza mafanikio katika sekta hii ya elimu, HakiElimu imeandaa
vipindi vya radio katika mikoa ya Morogoro, Mbeya, Tabora, Tanga, Kagera,
Dodoma na Mara ambavyo vitatoa nafasi ya Marafiki wa Elimu kujadili jinsi
gani elimu ya awali inaweza kuboreshwa hapa nchini na nini kifanyike.
Katika vipindi hivyo vinavyoendeshwa na Marafiki wa Elimu wananchi wote
mnaombwa kupiga simu na kutoa mchango wa nini kifanyike ili kuboresha
elimu ya awali nchini.
- Hali
kadhalika, kwa watanzania wanaotumia mtandao wa Internet tunawaomba mshiriki
kampeni hii kwa kutembelea mtandao wetu wa facebook katika www.facebook.com/hakielimu,mtandao
wa twitter unaopatikana kupitia www.twitter.com/hakielimu
na blog yetu inayopatikana kupitia www.hakielimu.blogspot.com.
Sambamba na hilo, leo tarehe
27 Septemba, 2012, HakiElimu inazindua matangazo mawili ya radio na televisheni
yatakayokuwa yakiruka katika vituo vya radio na televisheni takribani 12 nchini
Tanzania. Moja ya matangazo hayo litaonesha
changamoto zilizoko katika elimu ya awali nchini na tangazo la pili litaonesha mfano
wa shule bora au elimu ya awali tunayoitaka nchini Tanzania. Tunaomba mtumie dakika zisizozidi 3 kuangalia
matangazo ambayo pia yanapatikana katika mtandao wetu wa YouTube kupitia www.youtube.com/hakielimutz
Imetolewa na
Bi.
Elizabeth Missokia
Mkurugenzi
Mtendaji – HakiElimu
27
Septemba 2012