Wednesday, June 13, 2012

Kaloleni Sekondari: Shule ya kata inayoonesha njia mkoani Arusha




 Ile dhana ya kwamba shule zote za kata ziko katika mazingira magumu na hazifanyi vema katika maendeleo ya elimu siyo inaanza kupingwa kwa vitendo,utafiti uliofanywa na mwandishi kutoka HakiElimu mkoani Arusha umegundua kuwa ingawa shule nyingi za kata hazifanyi vyema na kukabiliwa na changamoto lukuki, kuna baadhi ya shule za sekondari za Kata ambazo zina maendeleo mazuri kitaaluma kushinda hata zile shule Kongwe za Serikali na Shule nyingi za binafsi.

Mfano wa shule za kata zinazofanya vema ni shule ya sekondari ya kata ya Kaloleni iliyoko wilayani Arusha. Shule hii ilianzishwa mwaka 1998 ni moja ya shule zinazofanya vema kielimu ambapo katika mtihani wa kitaifa wa mwaka jana wa kidato cha nne , shule hii ilishika nafasi ya 12 kati ya shule 137 za mkoa wa Arusha zilizofanya mtihani huo na kushika nafasi ya 179 kati ya shule  3108 zilizofanya mtihani huo nchini  .Shule hii ilikuwa na jumla ya watahiniwa 179 waliofanya mtihani huo ambapo watahiniwa 15 walipata daraja la kwanza, 17 wakapata daraja la pili, 47 walipata daraja la tatu, 85 wakapata daraja la nne na 15 walifeli kwa kupata daraja 0.
Vibao mbali mbali kuonesha sehemu na huduma mbalimbali shuleni hapo



Baadhi ya magari ya walimu na wageni yakiwa yameegeshwa shuleni hapo kusubiri wamiliki wao wakiwa kazini

Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya sekondari Kaloleni, Mrs Machange M.J

Tofauti na shule nyingine za kata , shule hii ina maabara kwa ajili ya masomo ya sayansi ambapo mwandishi alifanikiwa kutembelea maabara za somo la Fizikia, Kemia na Bailojia. Pia jambo lingine la utofauti ni mazingira ya shule kuwa mazuri ikiwemo sehemu ya kuegeshea magari ya wafanyakazi na wageni ambapo mwandishi aliduwazwa na neema aliyoiona ya eneo hilo tofauti ya shule nyingine za kata zenye mazingira magumu. Hii huenda ikawa ni kutoka na mazingira ya shule hii kuwa katikati ya jiji la Arusha eneo la Kaloleni.
Maabara kwa shule ya sekondari ya Kaloleni si jambo geni kwani zipo maabara za kila somo la sayansi.hii ni maabara maalumu ya elimu ya viumbe (Baiolojia)

Maabara ya Chemistry

Maabara ya Physics



Pamoja na mafanikio hayo, shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mlundikano wa wanafunzi ambapo kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 967 wa kidato cha kwanza mpaka cha nne, huku kukiwa na idadi ndogo ya walimu na kulazimika kuajiri walimu waliohitimu kidato cha sita kuokoa jahazi. Pia shule hiyo ni moja ya shule zilizopokea wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika katika kidato cha kwanza ambapo jumla ya wanafunzi watatu walikuwa na maksi mbaya sana katika mtihani uliotolewa kwa kupata maksi chini ya tano katika mitihani iliyofanywa ya kuhesabu kusoma na kuandika kufuatia wimbi kubwa la wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika nchini kuchaguliwa kujiunga na masomo ya Sekondari jambo ambalo lilipigiwa kelele na wadau mbalimbali likiwemo shirika la HakiElimu.

Habari na picha zote na Abraham Lazaro alieyekuwa Arusha





0 comments:

Post a Comment

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More