Huu ni mfano wa kuigwa kwa shule zingine kwani kuwepo kwa mazingira na vifaa vya kufundishia kama vile Kompyuta kunarahisisha uelewa wa wanafunzi. Safi sana shule ya sekondari Mpunyule.
Shule tatu wilayani Kilwa zipo kwenye mpango wa kusaidiwa kompyuta na shirika lisilokuwa la kiserikali la UKENGEE FOUNDATION ambalo toka mwaka 2009, limesaidia zaidi ya wanafunzi 9,000 kusoma somo la TEHAMA kwa vitendo tofauti na shule zingine za serikali ambao husoma nadharia tuu.
Shule ya Sekondari Mpunyule ni shule ya kata, ina jumla ya kompyuta 20 zinazotumiwa na wanafunzi 264 wa kidato cha kwanza mpaka cha nne.Kutokana na shule kutokuwa na umeme, kompyuta hizi zinatumia umeme wa jua. Shule hii ipo kilometa 105 kutoka kilwa mjini.Hii ni mojawapo ya shule tatu za wilaya ya kilwa zenye vifaa hivi adimu kwa shule nyingi nchini. Shule zingine zenye kompyuta wilayani Kilwa ni Kilwa Day na Ilulu.
|
2 comments:
Hongera sana uongozi na wote waliofanikisha hilo
halafu ooh miaka hamsini hakuna kilichofanyika...jamani !
Post a Comment