Miaka 10 ya HakiElimu

Mgeni rasmi katika sherehe za miaka kumi ya hakiElimu ambaye ni Mh. Samuel Sita

Young Boys Carrying Sand in a Pull Cart After Attending School

Young boys carrying sand in a pull cart after attending school to earn probably stationery money at Midizini area in Manzese

>Mathematicians in the Making....

Samia Tajiri(right)of Kiwalani Primary School in Dar es Salaam does her mathematics homework using bottle caps at a street side

Wednesday, December 5, 2012

Walimu Sekondari Wacheza ‘Table Tennis’ Ofisini Korogwe


Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Bungu wakiwa katika ofisi za walimu 
kuzungumzia mafanikio na changamoto mbalimbali kitaaluma katika shule hiyo.
Ofisi ya Walimu Shule ya Sekondari Bungu.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Bungu, Dismas Kimweli (kushoto) akifanya 
mahojiano na Mhariri wa Thehabari.com, Joachim Mushi alipotembelea 
baadhi ya Shule za msingi na sekondari Halmashauri ya Korogwe juzi.

Habari na Thehabari.com na HakiElimu
WANAFUNZI wa Shule ya Sekondari Bungu iliyopo Korogwe Vijijini wamelalamikia kitendo cha baadhi ya walimu wao kucheza mchezo wa table tennis ofisini (staff room) tendo ambalo limekuwa likifanyika hata wakati wa kazi/vipindi vya masomo. Malalamiko hayo yametolewa juzi ambapo mwandishi wa Thehabari.com alitembelea shule hiyo kuangalia changamoto mbalimbali za elimu eneo la Korogwe Vijijini.
Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina yao kiusalama na mwandishi wa habari hizi baadhi ya wanafunzi hao walisema wapo walimu ambao wamekuwa wakicheza mchezo huo hata wanapokuwa na vipindi jambo ambalo huwakatisha tamaa wanafunzi. “Wapo baadhi ya walimu wamekuwa wakijisahau na kucheza table tennis hata kama ni muda wa vipindi…na endapo akiwaanacheza na kiongozi wa darasa asimfuate kumkumbusha kipindi anaweza asije kabisa,” alisema mmoja wa wanafunzi hao.
Thehabari.com ilifika shuleni hapo na kuingia hadi ofisi ya walimu (staff room) na kushuhudia meza ya table tennis ikiwa imefungwa katikati ya ofisi hiyo tena ikipewa nafasi kubwa zaidi ya vifaa vingine vya kikazi vya walimu hao.
Hata hivyo mwandishi wa habari hizi alipozungumza na Mkuu wa Shule ya Sekondari Bungu,Dismas Kimweli kutaka kujua sababu ya shule hiyo kuweka uwanja wa table tennis ofisini hapo mwalimu huyo alisema wameufunga kwa muda kutokana na kukosa eneo la kuuweka, lakini wanafanya jitihada za kuutoa uwanja huo.
“Ni kweli eneo hili kufungwa uwanja kama huo si sahihi…hili nalielewa lakini tuliufunga kwa muda tu na hivi sasa tunajiandaa kuuamisha,” alisema Kimweli. Akifafanua zaidi alisema kutofundishwa kwa baadhi ya vipindi kwa wanafunzi hakutokani na michezo ya table tennis shuleni bali uchache wa idadi ya walimu shuleni hapo. Alisema kutokana na uchache huo wa walimu baadhi ya mwalimu huwa na vipindi karibia 70 kwa wiki jambo ambalo huwazidi baadhi yao hivyo kujikuta wakitupiwa lawama.
Shule ya Sekondari Bungu iliyoanzishwa mwaka 1989 yenye jumla ya wanafunzi 640 ina walimu 12 tu huku kati ya idadi hiyo walimu watatu kwa wako masomoni.



Monday, November 26, 2012

Ukata unachangia uelewa finyu wa maudhui ya mtaala kwa walimu

Mkurugenzi wa Utafiti, Habari na Machapisho wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) 
Makoye Wangeleja akisisitiza jambo siku ya uzinduzi wa ripoti ya Utafiti
 Juu ya Uhusiano Uliopo Kati ya Mitihani na Mitaala


Imeelezwa kuwa ufinyu wa bajeti umekuwa ukikwamisha juhudi za kutoa elimu ya mitaala kwa walimu ili kuwajengea uwezo wa kuweza kuelewa maudhui yaliyomo kwenye mitaala ili kuwawezesha kuelewa na kuweza kutafsiri kwa vitendo maudhui ya mitaala katika ufundishaji.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Utafiti, Habari na Machapisho wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) Makoye Wangeleja wakati akichangia ripoti ya utafiti iliyowasilishwa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dr Kitila Mkumbo.

Wangeleja alisema TIE imekuwa ikishirikisha walimu kwa kiasi kidogo hali inayotokana na kutokuwa na fedha za kutosha kwaajili ya kazi ya kuwashirikisha walimu katika utungazi na kuwafundisha ili kuelewa vyema maudhui ya mtaala unaotumika.
 

Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti iliyofanywa na HakiElimu iliyofanya kwa ushirika wa Dr Kitila Mkumbo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ilieleza kuwa kwa mujibu wa mtaala wa elimu wa mwaka 2005 unaotumika sasa, mazoezi ya mwanafunzi shuleni yanatakiwa kuchangia nusu ya alama za mwanafunzi katika mtihani wa mwisho, lakini walimu hawaamini kama hali ndivyo ilivyo. 

Walimu walisema waziwazi kuwa iwapo alama za kwenye mazoezi zingetumiwa kwenye mtihani wa mwisho, kusingekuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaofeli mtihani kama tulivyoshuhudia hivi karibuni katika mfumo wetu wa elimu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya utafiti, idadi kubwa ya walimu hawana uelewa wa mahitaji ya mtaala na mazingira ya kufundishia na kujifunzia ni duni katika utekelezaji bora wa mtaala.Hali ambayo Wangeleja amesema inasababishwa na ufinyu wa bajeti katika kutekeleza mpangowa kutoa elimu ya mitaala kwa walimu wote nchini.

Utafiti huo umezidi kubainisha kuwa ingawa maudhui ya mtaala wa elimu yanaonekana kuwa ni yale ya kumjengea mwanafunzi ujuzi, taratibu za tathmini hazifuati falsafa hiyo. Kwa mujibu wa mtaala wa elimu, mazoezi na maendeleo ya kawaida ya shuleni yanatakiwa kuchangia asilimia 50 za alama ufaulu na asilimia 50 ndio zinatoka kwenye mtihani wa mwisho suala ambalo utafiti umelitilia mashaka kwani hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa baraza la mitihani linatumia falsafa hiyo.

Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya HakiElimu, Marjorie Mbilinyi 
akifuatilia ripoti ya utafiti iliyozinduliwa leo HakiElimu.Pembeni ni Meneja wa Idara ya Utawala na Fedha ya HakiElimu Daniel Luhamo
"Falsafa mojawapo ya mitaala inayozingatia ujuzi na uwezo wa mhitimu ni kutoa kipaumbele kilichosawa kati ya mitihani ya mwisho na mitihani ya mashuleni, Kulikuwa na taarifa za kukanganya kuhusu mchango wa mazoezi kwenye alama ya mwisho ya mwanafunzi" alisema Dr Kitila Mkumbo wakati akiwasilisha ripoti ya utafiti huo mbele za wandishi wa habari..

Kwa miaka mitano mfurulizo hasa miaka ya 2010 na 2011 ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne katika mitihani ya taifa alishuka kwa kiwango cha kutisha kwa wanafunzi wengi zaidi ya asilimia 80 wakipata daraza la nne na sifuri. Mfano katika wanafunzi 354042 waliofanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne mwaka 2010, wanafunzi 117,021walipata daraja sifuri ikiwa ni asilimia 50 ya watahiniwa wote, wanafunzi 136,633 ambao ni asilimia 38.6 walipata daraja la nne na kufanya asilimia 88.6 ya watahiniwa wote kupata daraja la nne na sifuri. ni wanafunzi 15,335 sawa na asilimia 4.3 ndio waliopata daraja la kwanza na la pili.





Friday, November 23, 2012

Utafiti: Uelewa finyu wa mitaala chanzo cha matokeo mabaya ya mitihani


 Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dr Kitila Mkumbo 
akitoa matokeo ya utafiti katika ukumbi wa mikutano wa HakiElimu.
 Imebainika kuwa matokeo mabaya kwenye mitihani ya taifa hayahusiani na kutofautiana kati ya mitihani na maudhui ya mtaala ingawa, uelewa finyu wa walimu juu ya maudhui ya mtaala wa elimu ndicho chanzo cha matokeo mabovu ya mitihani ya taifa.

Pia imebainika kuwa mtaala wa elimu unatekelezwa kwa kiwango duni kwa kuwa idadi kubwa ya walimu hawaelewi mahitaji ya mtaala na mazingira ya kufundishia na kujifunzia ni duni katika utekelezaji bora wa mtaala.
Hayo yamo katika ripoti mpya ya utafiti uliofanywa na HakiElimu kwa kushirikiana na Dr Kitila Mkumbo wa chuo kikuu cha Dar es Salaam wenye kichwa cha habari 'Uhusiano kati ya Mitihani na Mitaala,' utafiti huo ulikuwa na lengo la kujibu swali Kuu: Je, Wanafunzi Wanafeli Mitihani au Mitihani Inawafelisha Wanafunzi?

Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya HakiElimu, Marjorie Mbilinyi 
akifuatilia ripoti ya utafiti iliyozinduliwa leo HakiElimu
"matokeo duni katika mtihani wa taifa yanatokana utekelezaji duni wa mtaala kuliko mitihani yenyewe, Inaonekana kwamba, japokuwa Serikali imekuwa ikitekeleza mtaala unaomjengea mwanafunzi ujuzi tangu 2005, ni walimu wachache wanaoifahamu dhana na falsafa ya mtaala huu"Alisema Dr Mkumbo

Utafiti huo umezidi kubainisha kuwa ingawa maudhui ya mtaala wa elimu yanaonekana kuwa ni yale ya kumjengea mwanafunzi ujuzi, taratibu za tathmini hazifuati falsafa hiyo. Kwa mujibu wa mtaala wa elimu, mazoezi na maendeleo ya kawaida ya shuleni yanatakiwa kuchangia asilimia 50 za alama ufaulu na asilimia 50 ndio zinatoka kwenye mtihani wa mwisho suala ambalo utafiti umelitilia mashaka kwani hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa baraza la mitihani linatumia falsafa hiyo.

"Falsafa mojawapo ya mitaala inayozingatia ujuzi na uwezo wa mhitimu ni kutoa kipaumbele kilichosawa kati ya mitihani ya mwisho na mitihani ya mashuleni, Kulikuwa na taarifa za kukanganya kuhusu mchango wa mazoezi kwenye alama ya mwisho ya mwanafunzi" alisema Mkumbo.

Ripoti hiyo ilizidi kueleza kuwa mmoja wa maafisa wa mtihani aliyesailiwa alisema waziwazi kuwa mazoezi yanachangia nusu ya alama za mwanafunzi katika mtihani wa mwisho, walimu walikuwa hawaamini kama hali ndivyo ilivyo. Walimu walieleza kuwa iwapo alama za kwenye mazoezi zingetumiwa kwenye mtihani wa mwisho, kusingekuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wanaofeli mtihani kama tulivyoshuhudia hivi karibuni katika mfumo wetu wa elimu.
Meneja katika idara ya utafiti na uchambuzi wa sera wa HakiElimu Boniventura Godfrey 
akifafanua jambo.Kushoto ni Meneja wa idara ya habari na utetezi Ndugu Nyanda Shuli

Meneja wa idara ya utawala na fedha Daniel Luhamo akiwa na Mwenyekiti 
wa bodi ya HakiElimu Bi Illuminata Tukai wakifuatilia matokeo ya utafiti

Kwa miaka mitano mfurulizo hasa miaka ya 2010 na 2011 ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne katika mitihani ya taifa alishuka kwa kiwango cha kutisha kwa wanafunzi wengi zaidi ya asilimia 80 wakipata daraza la nne na sifuri. Mfano katika wanafunzi 354042 waliofanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne mwaka 2010, wanafunzi 117,021walipata daraja sifuri ikiwa ni asilimia 50 ya watahiniwa wote, wanafunzi 136,633 ambao ni asilimia 38.6 walipata daraja la nne na kufanya asilimia 88.6 ya watahiniwa wote kupata daraja la nne na sifuri. ni wanafunzi 15,335 sawa na asilimia 4.3 ndio waliopata daraja la kwanza na la pili.









Friday, November 16, 2012

Hali mbaya ya miundombinu ya shule wilayani Nyasa


Haya ni majengo ya vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Ndonga
 iliyopo Kata ya Kihagara wilayani Nyasa katika mkoa wa Ruvuma,  ambavyo viliezuliwa na
 kubomoka tangu 2011,wanafunzi wamekuwa wakisoma huku wakipigwa na jua na masomo husimama kipindi cha mvua

Mlundikano darasani, dawati linalopaswa kukaliwa na wanafunzi watatu ama wanne 
linatumiwa na wanafunzi watano. Hii ni Shule ya Msingi Ndonga iliyopo wilayani Nyasa


Hiki ni choo cha walimu kama kinavyoonyeshwa na mwalimu









Wednesday, October 10, 2012

Ben Pol aonesha kuwa msanii ni kioo cha jamii


Ben Pol msanii wa bongo flavor na mshindi wa tuzo za muziki za Kilimanjaro 
kwa mwaka 2011 na 2012 akiwa na bango la 'Boresha Chekchea'.

 Ule usemi wa kuwa msanii ni kioo cha jamii unajidhirisha kwa msanii wa mziki wa bongo flavor Bernard Michael Paul Mnyang'anga anae julikana kisanii kama Ben Pol kuunga mkono kampeni ya kuboresha elimu ya awali Tanzania.

Kampeni hiyo ilizinduliwa na HakiElimu tar 27 September 2012 iliyoambatana na uzinduzi wa matangazo mawili ya Television na redio kwaajili ya kuendeleza kampeni hii ya elimu ya awali iliyopewa jina la Chekechea.Matangazo hayo yanaonesha changamoto zilizoko katika elimu ya awali nchini na kutoa mfano wa shule bora au elimu ya awali inayotakiwa nchini Tanzania
 
Ben Pol akiwa katika baadhi ya kazi zake za kisanii jukwaani

 
Elimu ya Awali ni muhimu kwa maendeleo ya mtoto kimwili, kiakili na kimaadili. Katika Sera ya Elimu na mafunzo ya mwaka 1995 Serikali inaonesha umuhimu wa elimu ya awali,inapotamka ; “Tafiti kadhaa zilizofanyika nchini katika miaka ya 1980 zilibaini kuwa watoto waliopitia elimu ya awali huwa na mafanikio makubwa zaidi wanapoanza darasa la kwanza. Kutokana na kutambua umuhimu huu, Serikali iliamua kuingiza Elimu ya Awali kwa watoto wenye umri wa miaka 5 na 6 kwenye mfumo rasmi wa elimu na kila shule ya msingi inapaswa kuwa na madarasa ya Elimu ya Awali.”
Sera ya Elimu na Mafunzo 2010. Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi . Toleo jipya Rasimu ya 2 March 2011.(uk 5-6).

Uwekezaji katika huduma bora kwa mtoto na elimu ya awali huwa na faida maradufu kwa watoto wetu- ambao ni raia wetu wa  baadaye. Walipa kodi nao pia hufaidika na huimarisha uchumi. Faida ya uwekezaji wa fedha za umma katika elimu bora ya awali ni kubwa sana. Lakini je, Tanzania imeligundua hili na kulitekeleza kikamilifu?  Na je, maneno haya ambayo sera inasisitiza yako yanatekelezwa kwa vitendo?



Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More